Masha cha Utundu

Masha ni mtoto. Ni mwanafunzi hajui kusoma. Anajifunza sasa lakini mtundu.

Hili ni darasa la watoto. Huyu ni mwalimu hawa ni watoto ni mwanafunzi.

Pili si mtundu ni mpole. Anasema "mwalimu Masha mchokozi".

Pili analia mwalimu anasema nyamaza Pili anamwita Masha. Njoo hapa.

We Masha mtundu sana mtoto mtundu hawezi kusoma acha utundu.

Masha anasema ndiyo mwalimu. Mwalimu anafurahi sasa Masha ameacha utundu.

Watoto wanacheza. Wanacheza pamoja. Pili anacheza. Juma anacheza. Masha anacheza pia.

Wanacheza wanafurahi ni mchezo gani? Wanapenda Ukuti wanafurahi sana.

Loo, Masha anaanza anamvuta Juma anaanguka puu! Masha anacheka hajaacha utundu.

Mwalimu anakuja. Anakuja mbio. Nini Juma. Juma analia Masha kaniangusha.

Mwalimu anakasirika anamkemea Masha. Wewe mtoto mbaya. Masha anasema nimekosa mwalimu.

Mwalimu anafurahi. Basi nimekusamehe kengele inalia. Watoto wanafurahi wanarudi nyumbani. Kwa heri Mwalimu!

Masha amerudi. Amerudi nyumbani ametoka shuleni. Amechoka sana njaa inauma.

Shikamoo mama. Mama anaitikia marahaba Masha pole sana najua umechoka.

Huyu ni Zamda mdogo wake Masha. Haendi shuleni ananyonya maziwa.

Masha anasema we Zamda. Hujui kusema. Hujui kusoma. Nipe mimi maziwa.

Mama anafiki loo, we Masha! Huo sio utundu ni balaa leo nitakuchapa.

Basi mama, nimekoma. Nitaacha utundu. Usinichape. Mama hakumchapa.

Mama anapika. Anapika samaki. Baba na mama wanapenda samaki. Watakula samaki leo.

Masha! Mamaanaita. Bee Mama! Njoo upesi anakujua.

Mama anasema nataka pilipili. Nataka nyanya na ndimu mbili lete upesi.

Masha hachelewi. Analeta pilipili. Analeta nyanya na ndimu moja. Moja anaficha.

Anampa mama. Mama anapokea. Anatazama. Anashangaa. Anamtazama Masha.

Pilipili zipo. Nyanya zipo. Ndimu moja haipo. Iko wapi? Sijui mama.

Masha anacheza ni mchezo gani? Huu ni mdako. Mama anakuja. Anamwona Masha. Anarusha ndimu. Anadaka loo, mtoto huyu!

Mama anakasirika. Anaishika ndimu. Anamshika Masha. Anamchapa kidogo. Anamchapa tena.

Acha utundu, Mama anasema. Masha analia. Nisamehe mama. Nitaacha utundu.

Ewe Masha, ewe Masha. Acha utundu. Ukiwa darasani. Maaaasha! Acha utundu.

Ukiwa unacheza. Wewe na wenzako. Usiwe mkorofi kwa utundu wako. Masha acha utundu. Ukirudi nyumbani. Msalimie mama. Msalimie baba. Usimfinye Zamda. Maaasha acha utundu.

Mama akikuita. Akiwa jikoni utike bee. Ukimbie mbio. Maasha acha utundu. Masha anasema, "mimi si mtundu. Najua kusoma. Najua kuchora. Anagalia hapa. Huyu ni Mwalimu."